Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 02:06

Mtoto wa rais wa Uganda Yoweri Museveni anataka kumrithi babake ikulu


Jenerali Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa rais wa Uganda Yoweri Museveni

Mtoto wa rais wa Uganda Yoweri Museveni, Generali Muhoozi Kainerugaba, ametangaza kwamba atagombea urais na kumrithi babake.

Muhoozi, ambaye amekuwa kamanda wa kikosi maalum cha jeshi chenye majukumu maalum, na kuwa kamanda wa wanajeshi wa ardhi kabla ya kupandishwa cheo na kuwa generali.

Muhoozi amesema kwamba atagombea urais kama ishara ya kutoa heshima kwa mamake, Janet Museveni.

Janet Museveni, mke war ais Museveni, ni waziri wa elimu nchini Uganda.

“Mama yangu ni kama Malaika. Ni mama mwadhilifu sana ambaye kila mwanamme angependa kumuita mama” Amesema Muhoozi.

Mnamo mwezi Mei, wakati wa maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwake, Muhoozi alisema kwamba “maadui wametupiga vita sana kwa mda mrefu. Wametutusi kwa kutumia kila aina ya matusi. Hawaamini kwamba tumechukua udhibithi wa nchi. Tutaendelea hadi tuongoze hii nchi.”

Katika sherehe hizo zilizofanyika katika ikulu ya rais ya Entebbe, Janet Museveni alionekana kuidhinisha hatua ya Muhoozi kugombea urais, akisema kwamba “Mungu akuongoze katika safari hii ambayo umeanza.

Ili kugombea urais, itambidi Generali Muhoozi kujiuzulu kutoka kwa jeshi.

Uchaguzi mkuu utaandaliwa mwaka 2026.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG