Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 21:14

Mtoto wa Rais wa Comoro kuchukua nafasi ya baba yake


Rais wa Russia Vladimir Putin akipeana mkono na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, ambaye ni Rais wa Comoro Azali Assoumani huko Saint Petersburg, Julai 28, 2023. Picha na REUTERS

Picha na video za Ibrahim Youssouf Azali, kijana na mwenye utashi, ambaye ni mtoto wa Rais wa Comoro Azali Assoumani yuko tayari kabisa akisubiri kuchukua madaraka.

Wakati chama tawala cha visiwa hivyo vidogo katika bahari ya Hindi kilipokutana kwa ajili ya kumteua katibu mkuu mpya mwishoni mwa wiki, wengi wao walidhani nafasi hiyo ya juu angepewa Nour El Fath Azali mwenye umri ya miaka 39.

Azali mwenyewe -- kwa sasa ni mshauri binafsi wa baba yake – amekuwa akionekana yuko tayari kuchukua jukumu kubwa zaidi.

"Kama chama kitaniomba, nitakubali uamuzi wao," Azali aliliambia shirika la habari la AFP, pembeni mwa mkutano huo uliokuwa ukifanyika katika mji mkuu wa Moroni, Azali alikuwa amevaashati jeupe na kofia ya bluu yenye nembo ya chama tawala.

Huku baba yake akitarajia kubaki madarakani kwa muhula mwingine wa miaka mitano baada ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwakani, baadhi yao wanaamini uteuzi wa Azali ungeweza kuahirishwa.

Azali, ambaye anajieleza kuwa ni "mtu anayependa ukamilifu", amefurahia kuongezeka kwa uwepo wake wa umma tangu baba yake, ambaye kwa sasa ni mkuu wa Umoja wa Afrika, aliyeshinda uchaguzi uliokuwa na utata mwaka 2019.

Kama mshauri wa rais mara nyingi anaonekana akiwa pamoja na mawaziri katika televisioni kwenye mikutano na waandishi wa habari, na yeye ndiye aliyekuwa msukumo wa kongamano la CRC lililofanyika katika hoteli ya Moroni, na kujionyesha kuwa na shughuli nyingi.

Ukizingatia historia na misukosuko ya visiwa vya Comoro na kile ambacho wakosoaji wanasema ni mwelekeo ya utawala wa kimabavu wa rais Assoumani, wengi wanaamini kuwa yuko tayari kutwaa madaraka ya nchi hiyo ndogo yenye watu wasiozidi milioni moja.

Assoumani anatarajiwa kwa kiasi kikubwa kuwania muhula mwingine mwakani, huku duru ya kwanza ya upigaji kura ikiwa imepangwa kufanyika Januari.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG