Mtetemeko huo ulitokea wakati wa mchana Jumanne na idara ya Jiolojia ya Marekani imeleza kwamba kitovu cha mtetemeko kilikuwa katika mji waMineral, jimbo la Virgina, km 135 kusini magharibi ya Washington. Huu ulikuwa mtetemeko mkubwa kuwahi kutokea Virginia tangu mwaka 1897.
Maafisa wa usalama waliamrisha watu kutoka kwenye majengo ya bunge, Pentagon na majengo megine ya serikali ikiwa ni pamoja na makao makuu ya VOA Washington, ambayo ilisitisha matanagzao yake kwa muda.
Mtetemko ulitikisa takriban miji yote ya pwani ya mashariki ya Marekani hadi Boston upande wa kaskazini mashariki ikiwa ni pamoja na Martha Vineyard Massachusetts ambako rais Barack Obama yuko likizoni. Mifumo ya usafiri kuanzia New York hadi hapa Washington ilisita kwa muda na kuanza kazi baada ya saa kadhaa.