Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 21:40

Mtayarishaji wa muziki wa Puerto Rico, Jose Hernandez afariki katika ajali ya ndege

Ndege aina ya Gulf stream 550 katika eneo la Yokota Japan ambayo hubeba watu wa hali ya juu.

Kampuni moja ya usafiri wa anga inasema ndege ndogo inayoimiliki  ilianguka huko Jamhuri ya Dominika ilipokuwa ikijaribu kutua dakika chache baada ya kuanza safari ya kuelekea Florida, na kusababisha vifo vya watu wote tisa, akiwemo mtayarishaji wa muziki kutoka Puerto Rico, Jose Angel Hernandez.

Helidosa Aviation Group inasema kwenye akaunti yake ya Twitter kwamba ndege hiyo ya Gulfstream ilikuwa imebeba wanahewa wawili na abiria saba ilipoanguka Jumatano. Inasema ndege hiyo ilikuwa imeondoka kwenye uwanja wa ndege wa El Higuero kuelekea Orlando, Florida, muda mfupi kabla ya kutaka kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Las Americas mji mkuu wa Jamhuri ya Dominika.

Kampuni hiyo haijatoa maelezo yoyote kuhusu ni kwa nini marubani walibatilisha safari ya ndege hiyo au sababu zinazowezekana za ajali hiyo. Uwanja wa ndege ulifunga shughuli zake baada ya ajali hiyo , na kuahirisha mamia ya safari za ndege.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG