Hatua hiyo imezidisha mzozo wa miezi kadhaa kati ya Musk na Mahakama ya Juu Brazil kuhusu uhuru wa kuzungumza, akaunti zenye mrengo wa kulia na upotoshaji wa habari. Jaji Alexandre de Moraes aliamuru siku ya Ijumaa kusimamishwa kwa mtandao huo.
Ili kuifungia X, mdhibiti wa mawasiliano wa Brazil, Anatel, imewaambia watoa huduma ya Internet kuzuia fursa ya ufikiaji katika miandao wa kijamii. Mpaka kufikia saa sita usiku, waendeshaji wakuu walishaanza kufanya hivyo.
De Moraes alimuonya Musk siku ya Jumatano usiku kuwa X inaweza kuzuiwa nchini Brazil endapo atashindwa kutekeleza agizo lake kumteua mwakilishi, na kutoa saa 24. Kampuni hiyo haikuwa na mwakilishi tangu mwanzoni mwa mwezi huu.
Jaji amesema jukwaa litaendelea kuzuiliwa mpaka litakapotekeleza maagizo yake, na pia kuweka faini ya kila siku ya dola 8,900 kwa watu au makampuni watakaoufikia mtandao huo kwa kutumia VPN.
Forum