Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 16:54

Maktaba ya umma ya Kenya kutumia mtandao


Maktaba ya umaa ya Kenya itaanza kutoa huduma za bure za kutumia mtandao kwa zaidi ya wanachama wake nusu milioni kuanzia mwezi huu.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kampuni ya 'Liquid Telecom Kenya,' pamoja na mamlaka ya mawasiliano ya Kenya, kuunganisha pamoja matawi yote 46 ya huduma za maktaba ya Kenya kwa mara ya kwanza.

Kila tawi ya maktaba hayo yote 46 litakua na komputa 1, pamoja na chombo cha Kindle na tablet kwenye program hiyo itakayogharimu shilingi milioni 72 na inayokusudia kutoa huduma za mtandao kwa watumizi wa maktaba aidha kwa kutumia komputa za maktaba au zao binafsi.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya 'Liquid Telecom Kenya,' Ben Roberts, amesema haja ya kutumia mtandao nchini Kenya imeongezeka kwa kiwango kikubwa na ina maana kwamba sasa kila mmoja ataweza kupata huduma hiyo kwenye maktaba za kitaifa.

Huduma zinazotarajiwa kutolewa kupitia mtandao ni kama zile za kiserikali, utafiti na pia nafasi za ajira. Huduma hizo zitatolewa bure kwa watoto wa chini ya miaka 14 na shilingi 20 kwa watu wazima. Mikakati ya kiusalama pia imewekwa kuhakikisha kuwa mtandao hatumiki vibaya.

Kwa wastani kila tawi la maktaba huwa na watumiaji elfu 10 kwa mwaka, na katika makao makuu ya Nairobi kuna watu laki moja hutumia huduma za makao hayo.

XS
SM
MD
LG