Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 11:24

Msumbiji yatangaza kisa cha maambukizi ya polio


Mtoto akipokea chanjo ya polio katika mji wa Lilongwe Malawi, March 20, 2022.
Mtoto akipokea chanjo ya polio katika mji wa Lilongwe Malawi, March 20, 2022.

Msumbiji imetangaza kisa cha maambukizi ya virusi vya polio baada ya kugunduliwa katika mtoto anayeishi katika eneo la Tete, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Shirika la afya duninai WHO limesema kwamba kisa hicho ni cha kwanza kuripotiwa katika kipindi cha muongo mzima.

Hiki ni kisa cha pili cha polio kusini mwa Afrika, baada ya Malawi kuripoti maambukizi mnamo mwezi Februari.

Mkurugenzi wa WHO Afrika, Matshidiso Moeti, amesema kwamba kugunduliwa kwa maambukizi hayo ya polio ni hatua inayoleta wasiwasi mkubwa, na dhihirisho kwamba virusi hivyo hatari vinasambaa kwa kasi.

Ugonjwa wa polio hushambulia mfumo wa neva na unaweza kusababisha ulemavu baada ya mda mfupi.

Polio hauna tiba lakini maambukizi yanaweza kuzuiwa kwa kutolewa chanjo.

XS
SM
MD
LG