Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 18:38

Msumbiji yakabiliwa na ukame wa chakula


Wakulima katika shamba la mahindi
Wakulima katika shamba la mahindi

Takribani watu milioni 1.5 kwenye maeneo ya kati na kusini mwa Msumbiji wanakabiliwa na ukame kutokana na hali ya El Nino na hali hiyo imekuwa ikiendelea kwa miezi kadhaa sasa.

Ripoti kutoka kwa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia maswala ya kibinadamu-OCHA, inasema hali ya ukosefu wa chakula nchini humo imeanza kuathiri watoto.

Msemaji wa OCHA, Jens Laerke, alisema kuwa takriban watoto 95,000 wanakabiliwa na upungufu wa lishe bora. Aliiambia VOA kuwa hali hiyo huenda ikapelekea vifo katika kipindi cha miezi 6 ijayo iwapo hawatapata msaada wa lishe bora.

El Nino husababishwa na ongezeko la joto kwenye bahari ya Pacific huku hali hiyo ikiathiri msimu wa mvua. Umoja wa Mataifa umepokea dola milioni 13 pekee kati ya dola miloni 203 zinazohitajika kwenye operesheni nchini humo mwaka huu.

Learke alisema watu 423,000 walipata msaada wa chakula mwezi Aprili na Mei. Kutokana na upungufu wa fedha aliongeza kusema kuwa watu zaidi ya 100,000 kwenye idadi hiyo watakosa msaada mwezi huu.

XS
SM
MD
LG