Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:36

Msomali aliyefanya shambulizi Canada alitoroka Marekani


Abdulahi Hasan Sharif, mshukiwa wa shambulizi nchini Canada
Abdulahi Hasan Sharif, mshukiwa wa shambulizi nchini Canada

Mhamiaji mmoja raia wa Kisomali aliyeshutumiwa kumgonga na kumchoma kisu polisi wa Canada na kuwagonga watembea kwa miguu wane wengine aliwahi kuwekwa kwenye kizuizi cha Marekani na kufukuzwa nchini.

Abdulahi Hasan Sharif alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza huko Edmonton Jumanne siku tatu baada ya kushukiwa kufanya shambulizi. Anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya uhalifu ikiwemo makosa matano ya jaribio la mauaji.

Msemaji wa idara ya uhamiaji na forodha wa Marekani alisema Sharif alikuwa kwenye kizuizi cha ICE kwa miezi minne mwaka 2011 akisubiri utaratibu wa kurejeshwa nchini Somalia. Aliachiwa huku akiwa chini ya uangalizi lakini alishindwa kufika kukutana na maafisa wa uhamiaji mwezi Januari mwaka uliofuata. Badala yake Sharif alikimbilia Canada akitafuta hifadhi ya ukimbizi.

Polisi wa Edmonton wakichunguza tukio lililosababishwa na Sharif
Polisi wa Edmonton wakichunguza tukio lililosababishwa na Sharif

Maafisa wa Canada walimchunguza Sharif kwa shutuma za msimamo mkali mwaka 2015 lakini hawakupata ushahidi wa harakati za kihalifu. Anashutumiwa kumgonga ofisa polisi kwa gari lake nje ya uwanja wa mpira huko Edmonton siku ya Jumamosi kisha kumchoma kisu ofisa huyo mara kadhaa.

Sharif anashutumiwa pia kuwagonga watu wane akiwa kwenye gari akijaribu kukimbia kukamatwa na polisi. Sababu zilizopelekea shambulizi hilo bado hazijulikani lakini Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau aliliita tukio hilo ni kitendo cha kigaidi.

XS
SM
MD
LG