Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 27, 2022 Local time: 21:21

Msichana aliyetekwa nyara wa Chibok aokolewa


Mmoja wa wasichana wa shule waliotekwa na Boko Haram katika tukio lililotikisa dunia na utekwaji wa wasichana wengi kaskazini mashariki mwa Nigeria leo hii ameokolewa kwa mujibu wa msemaji wa jeshi na kiongozi wa kijiji.

Msichana huyu anakuwa ni wa kwanza kuokolewa toka wanamgambo wa kundi la Boko Haram kuvamia shule ya sekondari ya serikali katika mji wa Chibok mwezi Aprili mwaka 2014 na kukamata wasichana karibu 300.

Wengi wao walikimbia mara tu baada ya kutekwa lakini mpaka sasa wengine 200 hawajulikani walipo.

Taarifa zaidi kuhusu kuokolewa huko bado hazijatollewa. Msemaji wa jeshi Sani Usman amesema jeshi la Nigeria lilimuokoa msichana huyo katika kijiji cha Baale, karibu na mji wa karibu wa Damboa.

XS
SM
MD
LG