Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 22:22

Mshirika mkuu wa Imran Khan ajitoa serikalini


Waziri mkuu wa Pakistan Imran Khan na mkewe Jemima mjini Islamadad.(REUTERS/Mian Khursheed.
.
Waziri mkuu wa Pakistan Imran Khan na mkewe Jemima mjini Islamadad.(REUTERS/Mian Khursheed. .

Waziri mkuu wa Pakistan aliye matatani, Imran Khan, alipata pigo kubwa la kisiasa Jumatano wakati mshirika mwingine mkuu wa serikali yake ya muungano alipoamua kujiunga na vikundi vya upinzani vinavyotaka kumuondoa madarakani kupitia kura ya kutokuwa na imani naye iliyotarajiwa mapema wiki ijayo.

Chama cha Muttahida Qaumi Movement (MQM), mshirika mkubwa wa Khan katika baraza kuu la bunge, kilitangaza Jumatano kuwa kimejiuzulu kutoka kwenye baraza la mawaziri la serikali kuu baada ya kufikia makubaliano na vyama vya upinzani.

Wapinzani wa kisiasa wanamshutumu nyota huyo wa zamani wa kriketi mwenye umri wa miaka 69 kwa kutawala vibaya nchi na kusimamia vibaya uchumi na mambo ya nje, madai ambayo Khan anayakanusha vikali.

Chama cha Khan cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) kilishinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2018 lakini kilikosa kupata kura nyingi katika bunge la wanacahama 342, na kumlazimu kuunda serikali ya mseto kwa usaidizi wa washirika wa kisiasa, ikiwa ni pamoja na MQM. Mapema katika wiki, PTI ilipoteza uungwaji mkono wa mshirika mwingine wa kikanda, Balochistan Awami Party (BAP).

XS
SM
MD
LG