Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 19:34

Shambulizi la maafisa Lousiana lilikuwa limepangwa kitaratibu - Polisi


 AFP file photo (L) obtained July 8, 2016 shows Dallas sniper Micah X. Johnson. Screenshot (R) taken from his personal website shows Baton Rouge shooter Gavin Long, also known as Cosmo Setepenra.
AFP file photo (L) obtained July 8, 2016 shows Dallas sniper Micah X. Johnson. Screenshot (R) taken from his personal website shows Baton Rouge shooter Gavin Long, also known as Cosmo Setepenra.

Mkuu wa polisi katika jimbo la Louisiana, hapa Marekani, amesema kuwa shambulizi lililowaua maafisa watatu wa polisi katika mji wa Baton Rouge jana Jumapili, lilikuwa limepangwa.

Akizungumza na shirika la habari la CNN, Supritendent wa polisi, Kanari MIKE EDMONSON alimema kuwa mshukiwa huyo aliwalenga polisi kwa sababu alikuwa anakusudia kuwaua maafisa hao, na wengine ambao wangejitokeza.

Mtu aliyetekeleza mauaji hayo ametambuliwa kama mwanajeshi wa zamani wa Marekani.

Wakaazi wa mji huo wa Baton Rouge wamekuwa katika hali ya wasiwasi baada ya maafisa wa polisi kumpiga risasi na kumwuaa mtu mmoja mweusi mapema mwezi huu. Maafisa wa kijeshi wamesema kuwa Gavin Long kutoka mji wa Kansas, jimbo la Missouri, aliwaua maafisa hao watatu wa polisi, huku akiwa amajifunika uso wake, katika siku ya kuadhimisha miaka 29 tangu kuzaliwa kwake.

Long alihudumu kama mwanajeshi kutoka mwaka wa 2005 hadi 2010, na kupanda cheo hadi akawa Sajenti. Alitumika nchini Iraq kutoka mwaka wa 2008 hadi 2009. Baadhi ya maandishi yaliyokuwa kwenye ukurasa wake wa Twitter ni swali hili: “Ni wakati gani utasimama ili watu wako wasiangamizwe kama ilivyokuwa kwa Wamarekani asili?’

XS
SM
MD
LG