Mkuu wa polisi mjini Las Vegas, Joseph Lombardo, amewaambia waandishi wa habari kuwa mshambuliaji huyo alikuwa katika ghorofa ya 32 katika jengo la Mandalay Bay Casino, lilioko upande wa pili wa eneo la shambulizi.
Polisi wamemtambua mshambuliaji huyo kama Stephen Paddock, miaka 64, na wanaamini kwamba alifanya hivyo akiwa peke yake bila ya kushirikiana na mtu yoyote.
Mamlaka zimesema kuwa zinamhoji mwanamke mmoja ambaye anaaminiwa kuwa alikuwa anaishi na mshukiwa huyo.
Mshambuliaji huyo aliuuawa kwenye chumba chake cha hoteli na polisi wanasema wamegundua silaha kadhaa.