Gaidi asiyejulikana alilipua bomu wakati mwanadiplomasia wa Russia alipotoka nje na kutangaza majina ya raia wa Afghanistan wanaoomba visa ambao walikuwa kwenye foleni, vyombo vya habari vya serikali ya Russia vimeripoti, vikinuku wizara ya mambo ya nje na mashahidi.
Hatma ya mwanadiplomasia huyo haikufahamika mara moja. Msemaji wa polisi, Khalid Zadran amesema gaidi wa kujitoa muhanga aliendesha shambulio hilo lakini aliuawa na walinda usalama wa Afghanistan kabla ya kuwafikia aliwowalenga.
Facebook Forum