Wakosoaji wa serikali wanasema utawala war ais Kais Saied umekuwa wa kimabavu.
Kiongozi wa ngazi ya juu katika kundi la Ennahda Noureddine Bhiri, anazuiliwa na polisi katika mji mkuu wa Tunis baada ya kukamatwa akiwa nyumbani kwake.
Anshutumiwa kwa kuwa sehemu ya kundi linalopanga njama za kutatiza usalama wa Tunisia.
Wakili wa kiongozi huyo Ines Harrathi, ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa facebook kwamba wengine waliokamatwa no wakili Lazhar Akremi, ambaye ni mkosoaji mkubwa wa rais Saied, na mkurugenzi mkuu wa radio huru ya Mosaique, Noureddine Bouttar.
Maafisa wa serikali hawajatoa ripoti yoyote kuhusu ukamataji huo ulioanza wikendi.
Msako huo unajiri baada ya kufanyika uchaguzi wa bunge ambapo asilimia 11 pekee ya wapiga kura walishiriki.
Facebook Forum