Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 16:02

Mrepublikan Glen Youngkin ashinda uchaguzi wa gavana wa Virginia, Marekani


Glenn Youngkin, gavana mteule wa Virginia.
Glenn Youngkin, gavana mteule wa Virginia.

Katika ushindi mkubwa kwenye jimbo la Virginia ambalo kwa kipindi kirefu limekuwa lenye mwelekeo wa demokratik, Mrepublican Glenn Younkin alishinda katika kinyang’anyiro cha ugavana mapema Jumatano na kuwa mgombea wa kwanza Mrepublican kushika wadhifa huo wa jimbo lote katika kipindi cha miaka 12.

Youngkin mwenye umri wa miaka 54 alimshinda Mdemokrat ,Terry Mcauliffe, hatua iliyoleta mabadiliko makubwa katika jimbo hilo ambalo lilibadilika kuwa mrengo wa kushoto zaidi ya muongo mmoja uliopita na lilichukuliwa na rais Joe Biden mwaka jana kwa tofauti ya pointi 10.

“Sawa tumeshinda kiti hiki, ni furaha isyo kifani. kwanza kabisa , kwanza kabisa, nawashukuru nyote kwa kusubiri, kusubiri dakika chache muda mrefu kuliko tulivyotarajia. Chakula cha Kifungua kinywa kitatolewa baada ya muda mfupi.”

Youngkin alisema wakati akaiwahutubia wafuasi wake waliojawa na furaha mapema Jumatano.

Mwanasisa huyo aliahidi haraka kuboresha shule, kodi za chini, na kuleta kile alichokiita "siku mpya kwa ajili ya watu wa virginia."

XS
SM
MD
LG