Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 22:23

Mrepublican Donald Trump asema uchaguzi Marekani umeibwa


mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump
mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump

Alisema katika mtandao wake wa twitter kwamba utafiti wa taifa unaonyesha kwamba kampeni zake dhidi ya mgombea wa chama cha Demecratic Hillary Clinton bado zinakaribiana

Mgombea urais wa chama cha republican , Marekani – Donald Trump amesema Jumapili kwamba anapoteza uungwaji mkono wa wapiga kura wanawake lakini akalaumu vyombo vya habari kutangaza taarifa za wanawake wanaodai aliwanyanyasanya kingono zilizoathiri kuwa na mvuto kwa wapiga kura hao.

Alisema katika mtandao wake wa twitter kwamba utafiti wa taifa unaonyesha kwamba kampeni zake dhidi ya mgombea wa chama cha Demecratic Hillary Clinton bado zinakaribiana. “ aliongeza kuwa unaweza kuamini kwamba nimepoteza wapiga kura wengi wanawake kutokana na matukio yaliyotengenezwa, ambayo hayakuwahi kutokea.Vyombo vya habari vimeiba uchaguzi!

Utafiti wa kura za maoni uliotolewa jumapili na mashirika ya habari ya The washington Post na ABC unaonyesha kuwa Clinton anaongoza kwa asilimia 47 na Trump ana asilimia 43 .

XS
SM
MD
LG