Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 06, 2023 Local time: 20:17

Mpinzani mkuu nchini Senegal ahukumiwa kifungo cha nyumbani cha miezi sita


Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko

Mahakama ya Senegal Jumatatu imemhukumu kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko kifungo cha nyumbani cha miezi sita katika kesi ya rufaa ya kashfa inayomkabili, hukumu ambayo inaweza kukwamisha mpango wake wa kuwania urais mwaka ujao.

Sonko, mwenye umri wa miaka 48, alipata nafasi ya tatu katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2019 na ana nia ya kugombea tena mwaka 2024, lakini kesi mbili mahakamani zinaweza kumzuia asigombee.

Alihukumiwa kifungo cha nyumbani cha miezi miwili na kulipa faini kubwa mwezi Machi kwa kumkashifu waziri wa utalii Mame Mbaye Niang, na mahakama ya rufaa ya mjini Dakar iliongeza kifungo hicho hadi miezi sita jana Jumatatu, hukumu ambayo inaweza kupelekea Sonko asiruhusiwe kugombea.

Msemaji wa chama cha Sonko, Ousseynou Ly, na wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii walisema pia kuwa hukumu hiyo inaweza kukwamisha mpango wake wa kuwania uongozi kama itatekelezwa, lakini mawakili wa mwanasiasa huyo waliondoka mahakamani bila kujibu maswali.

Sonko hakuwepo mahakamani, baada ya kuonya kuwa hatafika tena mahakamani bila kuhakishishiwa kwamba usalama wake utalindwa.

XS
SM
MD
LG