Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 10:44

Mpatanishi wa nyuklia wa Iran kwenda Vienna kwa mazungumzo


Mpatanishi wa juu wa nyuklia wa Iran, Ali Bagheri Kani, anasafiri kwenda Vienna, Jumatano kufanya mazungumzo ya kuboresha mkataba wa nyuklia wa 2015 amesema msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran.

Msemaji huyo ameongeza kusema kwamba Tehran, ipo tayari kufikia makubaliano ambayo yatahakikishia haki zake.

Mwezi uliopita mwanadiplomasia wa juu wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrel, alisema kwamba alipendekeza mkataba mpya wakuboresha mkataba ambao Iran iliachana na mipango yake ya nyuklia ili kulegezewa vikwazo vyake vya kiuchumi.

Mwaka 2018, aliyekuwa rais wa Marekani, Donald Trump, aliachana na mkataba huo kwa kuuita usiokuwa madhubuti katika kuibana Iran, na kuweka vikwazo vikali na kuifanya Iran kuanza kwenda kinyume na mkataba iliyouingia.

Mkataba huo ulioneka kama umerejewa Machi baadaa ya mazungumzo ya miezi 11 baina ya utawala wa rais wa Marekani, Joe Biden, na Tehran.

XS
SM
MD
LG