Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 18:11

Iran yasema itaendelea kufanya majaribio ya makombora


jaribio la kombora Iran

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeonyesha wasiwasi wake kuhusu majaribio hayo yaliyozinduliwa ambayo Irai imesema itaendelea nayo kwa siku ya Jumanne na Jumatano.

Iran inasema mpango wake wa makombora pamoja na majaribio yake iliyoyafanya wiki hii hayavunji makubaliano ya nyuklia iliyoyafikia mwaka jana na kundi la mataifa sita yenye nguvu.

Chombo cha habari cha serikali kimemnukuu msemaji wa waziri wa mambo ya nje Hossein Jaberi-Ansari akisema Iran itaendelea na mpango wake na kwamba ni halali na wa kujilinda kwa uasili.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeonyesha wasiwasi wake kuhusu majaribio hayo yaliyozinduliwa ambayo Irai imesema itaendelea nayo kwa siku ya Jumanne na Jumatano.

Msemanji wa wizara hiyo John Kirby amesema watayaangalia majaribio hayo na kuchukuwa hatua sahihi kama itahitajika kwa kupitia Umoja wa Mataifa ama ya umoja. Kirby pia amesema waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry alizungumza suala hilo na waziri wa mambo ya nje wa Iran, Javad Zarif hapo jana.

XS
SM
MD
LG