Afisa huyo, akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kabla ya mazungumzo yao, amesema vikwazo vilivyosalia vinaweza kutatuliwa na kutakuwa na mikutano zaidi inayolenga kufikia makubaliano kati ya Israel na Hamas ndani ya wiki ijayo.
Wapiganaji wanaoongozwa na Hamas walivamia kusini mwa Israel, 7 Oktoba mwaka jana, na kuua watu 1,200 na kuchukua mateka 250, kwa mujibu wa Israel, na kusababisha vita ambapo zaidi ya watu 38,000 wameuawa Gaza, kwa mujibu wa wizara ya afya ya eneo hilo, ambayo haijatofautisha vifo vya wapiganaji na raia katika hesabu yake.
Forum