Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 22, 2025 Local time: 12:10

Mpango wa Kenya wa kupeleka polisi nchini Haiti wasitishwa kwa muda na mahakama


Mkuu wa polisi wa kenya Jenerali Japhet Koome akizungumza na wanahabari kwenye picha ya maktaba.
Mkuu wa polisi wa kenya Jenerali Japhet Koome akizungumza na wanahabari kwenye picha ya maktaba.

Mahakama moja nchini Kenya Jumatatu imesitisha kwa muda mpango wa serikali wa kutuma polisi nchini Haiti chini ya kikosi cha Umoja wa Mataifa kwa nia ya kurejesha utulivu kwenye taifa hilo la Caribbean lililojaa magenge.

Wiki iliyopita Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliidhinisha kikosi cha pamoja kitakacho ongozwa na Kenya nchini humo, wakati Nairobi ikiahidi polisi 1,000. Hata hivyo hatua hiyo ya mahakama imechukuliwa kufuatia kesi iliyowasilishwa na mwanasiasa Ekuru Aukot ambaye anasema hatua hiyo ni kinyume cha katiba na haiungwi mkono na sheria yoyote wala mkataba.

Aukot ambaye ni wakili na mmoja wa watu walioandika katiba ya 2010, amedai kuwa Kenya inapeleka polisi kwenye taifa la kigeni wakati ndani ya nchi kuna changamoto za usalama. Haiti taifa lililopo kwenye ukanda wa magharibi limeshuhudia misukosuko kwa miaka mingi, wakati magenge yakichukua udhibiti wa baadhi ya maeneo na kusababisha ukatili mkubwa dhidi ya raia, huku uchumi na mfumo wa afya vikiachwa katika hali mbaya.

Upelekaji wa polisi wa Kenya nchini humo bado haujakamilika, kwa kuwa unahitaji kuidhinishwa na bunge kwa mujibu wa sheria.

Forum

XS
SM
MD
LG