Mpaka huo ulikuwa umefungwa kwa karibu miaka sita kutokana na sababu za kisiasa na baadaye kutokana na janga la virusi vya Corona.
Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Burundi, waziri Albert Shingiro, amesema kwamba Burundi inaitaka Rwanda kuwarudisha watu waliokuwa wamepanga kutekeleza mapinduzi ya mwaka 2015.
Jaribio la mapinduzi la kutaka kumuondoa madarakani aliyekuwa rais wa nchi Pierre Nkurunziza. Jaribio hilo lilifeli.
Rwanda ilikuwa imetangaza kufungua mpaka wake na Burundi miezi kadhaa iliyopita.