Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 19:22

Moto waua 21 Ukanda wa Gaza


Watu wakiwa nje ya jengo lililowaka Jabaliya katika kambi ya wakimbizi Ukanda wa Gaza , Novemba 17, 2022.
Watu wakiwa nje ya jengo lililowaka Jabaliya katika kambi ya wakimbizi Ukanda wa Gaza , Novemba 17, 2022.

Moto ulizuka Alhamisi jioni katika Ukanda wa Gaza na kuua takriban watu 21, watawala wa Hamas wa eneo hilo walisema.

Tukio hilo linakuwa moja ya hali mabaya zaidi katika miaka ya hivi karibuni nje ya ghasia zinazotokana na mzozo wa Israel na Palestina.

Moto huo ulizuka katika jengo la ghorofa tatu katika kambi ya wakimbizi ya Jabaliya kwa mujibu wa kundi la wanamgambo wa Palestina Hamas.

Jeshi la Ulinzi la Raia huko Gaza, ambalo linaendeshwa na Hamas, lilihusisha chanzo cha moto huo na petroli iliyokuwa ikihifadhiwa kwenye jengo hilo.

Haikuweza kufahamika mara moja jinsi petroli hiyo ilivyowaka. Maafisa walisema uchunguzi unaendelea.

XS
SM
MD
LG