Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 16:40

Moto unateketeza misitu Ufaransa, Ugiriki, Ureno na Spain


Mtaalam wa kuzima moto akijaribu kuzuia moto unaoteketeza misitu nchini Ufaransa kusambaa July 17 2022. Picha: AFP
Mtaalam wa kuzima moto akijaribu kuzuia moto unaoteketeza misitu nchini Ufaransa kusambaa July 17 2022. Picha: AFP

Kiwango cha joto kimeongezeka sana nchini Uingereza na Ufaransa huku moto ukiendelea kuteketeza misitu kusini magharibi mwa Ulaya bila kuwepo ishara yoyote ya kuzima.

Watabiri wametoa tahadhari kwa idhara 15 za Ufaransa kutokana na kiwango cha juu cha joto, huku serikali ya Uingereza ikishutumiwa kwa kukosa kuweka mikakati ya namna ya kukabiliana na ongezeko la joto.

Watabiri wanasema kwamba Maisha ya watu na viumbe wengine yamo katika hatari kubwa.

Ongezeko la joto ambalo linasambaa likielea sehemu za kaskazini, ni la pili kutokea kusini magharibi mwa ulaya katika wiki za hivi karibuni.

Moto unaendelea kutekeleza misitu nchini Ufaransa, Ugiriki, Ureno na Spain. Maelfu ya ekari za misitu imeteketea huku watu na watalii wakihama sehemu hiyo.

Wanasayansi wamesema kwamba joto hilo linatokana na mabadiliko ya hali ya hewa, na wameonya kwamba kuna uwezekano wa matukio kama hayo Pamoja na ukame, kuongezeka.

"Tutakuwa na wakati mgumu katika siku za baadaye sio tu kwa sbabau ya kuongezeka kwa viwango vya joto bali pia kutokana na upepo kubadilisha mkondo. Hii ina maana kwamba baadhi ya sehemu ambazo hazikuwa na matukio ya moto kutetekeza misitu, zinaweza kushuhudia hali hiyo.” Amesema Marc Vermeulen, mkuu wa wazima moto wa Gironde

Maafisa nchini Uhispania wameripoti matukio 20 ya moto kuteketeza misitu, na ambayo yamekuwa vigumu kuyadhibithi.

Ekari 4,500 za moto zimeteketea kusini mwa Galicia, kaskazini magharibi mwa Uhispania.

Zaidi ya watu 16,000 wamelazimika kukimbia makwao, na vituo saba vya kuwapa watu makao ya dharura kuundwa kutokana na moto unaoendelea kuteketeza misitu na makao ya watu.

XS
SM
MD
LG