Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 03:29

Moto katika shule ya vipofu Uganda umeua watoto 11


Mama wa watoto waliofariki dunia katika tukio la moto wilayani Mukono, Uganda wakiomboleza. Okt 25 2022
Mama wa watoto waliofariki dunia katika tukio la moto wilayani Mukono, Uganda wakiomboleza. Okt 25 2022

Watoto 11 wamefariki dunia kufuatia tukio la moto katika shule ya wanafunzi vipofu katika mji wa Mukono, nchini Uganda.

Msemaji wa polisi katika maeneo ya Kampala Luke Owesingire, amesema kwamba moto huo umetokea saa saba usiku wakati wanafunzi walikuwa wamelala.

“Kufikia sasa, watu 11 wamefariki dunia kutokana na moto huo. Watu 6 wapo katika hali mahtuti wakitibiwa katika hospitali ya Herona,” amesema Owesingire.

Polisi wanachunguza kilichosababisha moto huo.

​
XS
SM
MD
LG