Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:45

Uchaguzi Ufaransa waonyesha tetemeko kubwa la kisiasa


Marine Le Pen na Emmanuel Macron
Marine Le Pen na Emmanuel Macron

Matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais Ufaransa yamethibitisha kuwepo tetemeko kubwa la kisiasa nchini Ufaransa.

Mgombea urais mwenye mrengo wa kati Emmanuel Macron na mgombea mzalendo, mwenye kupinga uhamiaji Marine Le Pen wanaelekea katika kinyang’anyiro cha kumpata mshindi katika wiki mbili.

Wachambuzi wa siasa wameelezea matokeo hayo ya uchaguzi kuwa ni tetemeko kubwa la kisiasa nchini Ufaransa.

“Katika kipindi cha mwaka mmoja, tumebadilisha kwa ukamilifu siasa za Ufaransa,” Macron amesema katika mkutano wa ushindi wake Jumapili usiku, wakati mpinzani wake, Marine Le Pen, amewaambia wafuasi wake wenye hamasa “Ni muda wa kuwakomboa wananchi wa Ufaransa.”

Ni kwa mara ya kwanza katika historia ya Jamhuri ya Ufaransa ya kisasa kwamba urais utashikiliwa na mwanachama kutoka katika chama ambacho sio cha asili, akielezea kuna hisia nzito dhidi ya utawala ambao unaweza hatimaye ukaamua iwapo Ufaransa itaendelea kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya au itafuata uhuru wake wa kujitoa kama ilivyokuwa kwa kutoka kwa Uingereza katika umoja huo na ilivyokuwa Marekani chini ya Donald Trump.

Matokeo ya mwisho yalionyesha Macron amenyakua asilimia 23.8 za kura na Le Pen ameshinda asilimia 21.5 za kura. Upigaji kura ulikuwa kwa asilimia 79. Mshindi anahitaji wingi wa kura. Na hilo litaamuliwa May 7.

Macron, ambaye ana umri wa miaka 39 mwenye mrengo wa kati wa kushoto ambaye aliwahi kuwa waziri wa uchumi na ni muumini wa Umoja wa Ulaya na bishara ya ndani, ameongoza kura za awali pamoja na kuwa anamafungamano ya karibu siku za nyuma na Rais Msoshalisti aliyepoteza umaarufu Francois Hollande. Kukubalika kwake katika kampeni ya mwaka mzima kumejikita kwa watu wenye maisha bora mijini, ambapo utandawazi umewanufaisha wengi wao.

Changamoto inayomkabili ni jinsi ya kuwaunganisha wafuasi wake wa mrengo wa kati na mrengo wa kushoto, wakiwemo wanachama wa chama cha kisoshalisti kilichosambaratika cha Ufaransa, na kuwashawishi wapiga kura kwamba hatokuwa katika nafasi hiyo ya urais kuendeleza sera za Hollande. Pia amepokea pongezi kutoka kwa maafisa wa Umoja wa Ulaya.

Macron atapambana na Le Pen na chama chake cha National Front, ambacho kinaushawishi mkubwa katika maeneo yaliokuwa na viwanda huko miaka ya nyuma nchini Ufaransa ambapo kuporomoka kwa ajira kumeongezeka, pamoja na kukatishwa tamaa na uchumi wa kisasa na mipangilio ya jamii.

Le Pen, ambaye anataka Ufaransa ijitoe kutoka Umoja wa Ulaya, amefanikiwa kushawishi idadi kubwa ya wafuasi wa zamani wa siasa za mrengo wa kushoto na kati.

Kwa wiki mbili zijazo, Le Pen anamatumaini ya kupata wafuasi zaidi kutoka mrengo wa kulia na kati, hasa wale ambao hawajapendezwa na kuwepo matabaka nchini humo.

“Ni wakati mwafaka kuwakomboa wananchi wa Ufaransa,” aliwaambia wafuasi wake katika mkutano wa Jumapili.

XS
SM
MD
LG