Chama cha Mostaqbal Watn, kinaongoza katika matokeo ya awali ya duru ya pili ya uchaguzi wa bunge nchini Misri.
Chama cha Mostaqbal Want, maana yake hali ya baadaye ya taifa, kinamuunga mkono rais Abdel Fattah al-Sisi, kimepata viti 284 katika bunge lenye viti 596 katika mfumo wa utawala ambapo mshindi anapata madaraka yote.
Viti vilivyosalia vitaamuliwa katika duru nyingine ya uchaguzi utakaondaliwa baadaye mwezi hu una mapema mwezi Desemba.
Rais Sisi ana mamlaka ya kuteua wabunge 28 moja kwa moja.
Wagombea kadhaa na vyama vya kisiasa, wamewasilisha malalamiko kwa tume ya uchaguzi, wakidai kuwepo wizi wa kura katika uchaguzi huo lakini madai yao yametupiliwa mbali.
Baadhi ya malalamiko yamewasilishwa mahakamani.