Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 01, 2023 Local time: 16:32

Maafisa wa usalama wa Panama wavamia ofisi za Mossack Fonseca


panama papers

Maafisa wa serikali huko Panama wamevamia ofisi za kampuni ya kisheria ya Mossack Fonseca ambayo inahusishwa na uvujaji wa akaunti za kigeni za baadhi ya viongozi wa ulimwengu.

Mwanasheria mkuu wa Panama amesema kwenye taarifa kuwa waendesha mashitaka pamoja na polisi wanatafuta ushahidi unaoweza kuihusisha ofisi hiyo na shughuli zisizo halali. Mossack Fonseca inalaumiwa kwa kusaidia ukwepaji kodi na ubadhirifu.

Maafisa hao walifika kwenye ofisi hizo Jumanne jioni kufanya upekuzi kupata ushahidi utakaounga mkono shutuma hizo, wakati huo huo kampuni hiyo imeandika kwenye mtandao wa Twitter kwamba inaendelea kushirikiana na mamlaka katika uchunguzi.

Mwanzilishi wa kampuni hiyo, Ramon Fonseca, amesema kwamba kampuni yake haijavunja sheria na wala hakuna nyaraka iliyoharibiwa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG