Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:34

Morsi apinduliwa


Mkuu wa jeshi nchini Misri, Abdel Fattah al-Sisi akihutubia muda mfupi kabla ya jeshi kupindua nchi July 3, 2013
Mkuu wa jeshi nchini Misri, Abdel Fattah al-Sisi akihutubia muda mfupi kabla ya jeshi kupindua nchi July 3, 2013
Jeshi la Misri limemwondoa madarakani Rais Mohammed Morsi aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia na kuteuwa kiongozi wa muda wa nchi baada ya maandamano makubwa yanayoipinga serikali.

Akitoa hotuba kwa njia ya televisheni Jumatano jioni, mkuu wa jeshi, Abdul Fatah Khalil Al-Sisi alisema katiba ya Misri imefutwa kwa muda na mkuu wa mahakama ya katiba ameteuliwa kuwa kiongozi wa muda nchini humo. Bw. Sisi alitangaza kwamba jeshi linaangalia watu wa Misri kufuatana na maandamano makubwa ya upinzani yalioyodai Rais Mohamed Morsi ajiuzulu.

Kufuatia hotuba ya kwenye televisheni Jumanne bw. Morsi alitoa taarifa kupitia akaunti yake ya Twitter, akiita hatua ya jeshi kuwa “mapinduzi kamili”. Aliwasihi Wamisri wote kupinga hatua hiyo ya jeshi lakini pia wadumishe amani.

Kiongozi mpya wa muda nchini Misri, Adli Mansour ana umri wa miaka 68 ni mkuu wa sheria katika mahakama ya juu ya katiba. Ataapishwa Alhamis.

Kama sehemu ya mustakabali wa baadye wa Misri, kiongozi huyo wa kijeshi amesema anataka uchaguzi wa urais na wabunge, jopo la kutathmini katiba na kamati ya mashauriano kitaifa. Alisema utaratibu huo umekubaliwa baina ya makundi kadhaa ya kisiasa. Pia aliwasihi wananchi wa Misri kujiepusha na ghasia.

Jeshi lilimpa bwana Morsi saa 48 kutatua matatizo ya kisiasa au kuwepo hatari ya jeshi kuingilia kati. Viongozi wa jeshi walisema wataweka “mwongozo” kama tofauti kati ya serikali ya Ki-islam na wapinzani wake hawatamaliza matatizo yao ifikapo Jumatano mchana ya tarehe tatu mwezi wa saba mwaka 2013. Tarehe hiyo ya mwisho ilipita muda wake bila ya hatua zozote kuonekana.

Bwana Morsi hakika alikataa wito wa kujiuzulu na aliapa kuendelea kubaki madarakani hata kama itamsababishia kifo chake. Pia alilalamika kufuatia vitisho vya jeshi na hatua yao ya kuingilia mzozo wa kisiasa.

Baruti zilipaa angani kwenye umati wa watu wanaocheza na kupeperusha bendera katika uwanja wa Tahrir Square mjini Cairo, kiini cha ghasia za mwaka 2011 ambazo zilizomtimua madarakani rais wa muda mrefu wa Misri Hosni Mubarak.

Katika muda wa wiki chache zilizopita maandamano yenye ghasia kati ya wafuasi na wapinzani wa bwana Morsi yameuwa takribani watu 40.
XS
SM
MD
LG