Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:37

Morocco na Qatar zahusishwa na ufisadi katika EU


Mwanadiplomasia mkuu wa Umoja wa Ulaya, Alhamisi aliapa kutovumilia kabisa ufisadi alipokuwa Morocco, ambayo imehusishwa na kashfa ya biashara ya ushawishi inayolitikisa Bunge la Ulaya.

Msimamo wa EU uko wazi, wa kuto stahamili kabisa rushwa, mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell alisema baada ya mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Nasser Bourita.

Ziara ya Borrell inakuja wiki kadhaa baada ya polisi wa Ubelgiji kuvamia sehemu kadhaa zinazotumiwa na wabunge wa Ulaya na maafisa wengine.

Katika uvamizi huo polisi walipata dola milioni 1.6 taslimu, uchunguzi wa vyombo vya habari vya Ubelgiji vimeihusisha Qatar na Morocco.

Washukiwa wanne wanazuiliwa, akiwemo mbunge wa Ugiriki, Eva Kaili.

Wakati huohuo maafisa wanasema wataondoa kinga kwa wabunge wengine wawili wanaotuhumiwa kuchukua hongo kutoka Qatar.

Nchi hiyo ya Ghuba imeonya kuwa uchunguzi huo unaweza kuathiri uhusiano wa kiuchumi kati ya Ulaya na Qatar, ambayo ni muuzaji mkuu anayeibukia wa nishati kwa EU wakati inajaribu kupunguza utegemezi wa Russia.

Muwakilishi wa Italia Andrea Cozzolino, na mwenzake wa Ubelgiji, Marc Tarabella, ndio washukiwa wa karibuni katika kashfa ya ufisadi ambayo imeitikisa Brussels.

Kashfa hiyo imetikisa EU wiki nzima.

XS
SM
MD
LG