Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 20, 2025 Local time: 10:14

Morocco: Mwanaharakati ahukumiwa kifungo cha miaka minne jela kwa kumtusi mfalme Mohammed

Mfalme Mohammed wa Sita ( kulia) na waziri mkuu Saad Eddine El Othman( katikati) wakihudhuria hafla ya utiaji saini wa makubaliano kati ya Morocco na kampuni kubwa ya Ufaransa inayotengeneza magari, kwenye kastri ya kifalme mjini Cassablanca, December 11, 2017. Picha ya AFP

Mahakama moja ya Morocco Jumatatu imemuhukumu kifungo cha miaka minne jela mwanaharati aliyemtusi Mfalme Mohammed wa sita kwenye mitandao ya kijamii, wakili wake amesema.

“Rabie Al Ablaq amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela kwa kumkashifu mfalme mtandaoni,” wakili Abdelmajid Azaryah ameiambia AFP.

Kesi hiyo ilifunguliwa tarehe 11 Aprili baada ya Ablaq kuchapisha mtandaoni “ kanda za video zinazokosoa ukosefu wa usawa kati ya jamii na ufisadi,” wakili huyo amesema.

“Nimeshangazwa na hukumu hiyo kwa sababu alitoa maoni yake tu. Sikuhisi kwamba alihujumu taasisi ya kifalme,” ameongeza.

Wakili Azaryah amesema mwanaharakati huyo na mwanahabari wa masuala ya kijamii, mwenye umri wa miaka 35, aliombwa kulipa faini ya dirham 20,000, sawa na dola 2,000.

XS
SM
MD
LG