Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 16:48

Morgan Tsvangirai afariki dunia


Morgan Tsvangirai

Kiongozi wa muda mrefu wa upinzani na Waziri mMkuu wa zamani wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, amefariki baada ya kuugua saratani ya utumbo kwa muda mrefu.

Mnamo mwezi Juni mwaka 2016 alielezea tatizo la kiafya lililokuwa linamkabili na hivyo kuzima matumaini yake ya kuwa kiongozi wa taifa hilo la kusini mwa Afrika.

Morgan Richard Tsvangirai alizaliwa machi 10, 1952 katika eneo la Gutu kwenye jimbo la Masvingo, alipanda kutoka katika kazi yake ya awali ya mwalimu wa shule, na kuwa mmoja wa wanasiasa maarufu na mwenye ushawishi mkubwa nchini Zimbabwe, na kutambuliwa na kuheshimiwa kikanda na kimataifa.

Ni mmoja wa watoto tisa wa Tsvangirai Chibwe Tsvangirai na Lydia Zvaipa. Tsvangirai alipata umaarufu wa kitaifa kutokana na shughuli zake za awali kama katibu mkuu wa umoja wa vyama vya wafanyakazi Zimbabwe (ZCTU) mwaka 1988, ambacho kiliongoza migomo ya kitaifa kwa ajili ya hali njema za wafanyakazi nchini Zimbabwe.

Tsvangirai mwenye hamasa na nguvu, aliwahi kuwa mwanachama wa chama tawala cha zanu-pf, na kuwa kiongozi mwenye nguvu katika umoja wa wafanyakazi ZCTU na kukiongoza kuelekea kuwa chama cha siasa mwaka 1999, yeye akiwa ni rais muanzilishi. Kwa takriban miaka 20 tangu kuundwa kwake, Tsvangirai na chama chake cha MDC ujumbe wao mkuu kwa rais Robert Mugabe ulikuwa ni mabadiliko, ambaye aliondoka madarakani novemba 2017.

Hata hivyo, zanu pf bado kimeshika hatamu za uongozi, na hivi sasa kinaongozwa na aliyekuwa makamu rais Emmerson Mnangagwa, Tsvangirai alishinikiza mabadiliko ya uongozi na kuwaahi wafuasi wake kuwa atakishinda chama cha ZANU-PF licha ya afya yake mbaya.

Nguvu ya Tsvangirai kama kiongozi wa upinzani ulibainika mapema michache baada ya kuunda chama cha MDC, ambacho kilishiriki katika uchaguzi wa bunge mwaka 2000 na kujipatia ushindi wa viti 57 dhidi ya vya zanu pf 62, ushindi ambao haukutarajiwa tangu zanu pf ichukue mamlaka ya nchi mwaka 1980.

Jaribio la Tsvangirai kuwania urais mar ambili , lilifuatiw ana shutuma za njama za kutama kumuua rais Mugabe, jambo ambalo lilipelekea kukamatwa kwake kwa tuhuma za uhaini. Baada ya kumshinda Mugabe mwaka 2002, Tsvangirai alijikuta akitiwa mbaroni mara kwa mara kwa shutuma za ghasia za kijamii na kesi ndefu ya uhaini kabla ya kufutiwa mashtaka mwaka 2004.

Mwaka 2007, mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mwingine uliokuwa na ushindani mkali, Tsvangirai alijikuta akishambuliwa zaidi na wana usalama, kwa kuhusika kwake katika maandamano dhidi ya serikali. Akiongea baada ya kuachiliwa, Tsvangirai aliishutumu vikali serikali kwa kuwakandamiza raia wake.

Mwaka 2008, alishiriki tena uchaguzi na iliripotiwa alishinda katika kinyang’anyiro cha kuwania urais akipata 47.9% ya kura dhidi ya Mugabe aliyepata kura 43.2%. Hata hivyo hakupata fursa ya kuongoza nchi kwa vile uchaguzi ulirejewa na hapo ndipo Mugabe akaibuka mshindi katika duru ya pili ya uchaguzi.

Baada ya Mugabe kushinda hapo ndipo Tsvangirai na chama chake walitafuta usuluhisho wa kieneo ambao waliingilia kati na hatimaye makbaliano ya kisiasa yakafikiwa chini ya uongozi wa mkuu wa SADC ambaye alikuwa rais wa Afrika Kusini wakati huo, Thabo Mbeki nakufungua njia ya kuundwa kwa serikali ya kushirikiana madaraka kati ya MDC na Zanu-PF.

Tsvangirai ameacha mke, Elizabeth na watoto kadhaa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG