Pamoja wa jeshi la Congo, FARDC, MONUSCO, Jumatatu iliandaa ziara kwa wanahabari kutoka Goma, mji mkuu wa jimbo, kwenda mji wa Sake, ulilopo kilometa 25 kaskazini magharibi ya goma ndani.
MONUSCO katika vilima na mabonde karibu na kijiji cha Kimoka, ilifanya mazoezi bila kutumia risasi za moto. Mkuu wa oparesheni za MONUSCO, meja Eric Deshaies-Martin, amesema ni nafasi ya kiulinzi kuzuia kundi la M23 kusonga mbele.
Ijumaa kamanda mkuu wa kikosi hicho Otavio Rodrigues de Miranda, na FARDC, walitangaza kuanza kwa oparesheni yao ya pamoja “Springbok” ya kulinda watu na kuzuia M23 wasiutwae mji wa Goma.
Forum