Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 28, 2022 Local time: 02:57

Monusco waondoka Butembo kwa muda


Waandamanaji wakivamia ofisi za walinda amani wa Umoja wa Mataifa mashariki mwa Congo. July 25, 2022. REUTERS/Arlette Bashizi.

Tume ya Umoja wa Mataifa ya ulinzi wa amani nchini DRC imeondoka  katika moja ya miji  mikubwa mashariki  mwa nchi baada ya  maandamano mabaya dhidi ya kushindwa  kwake kuwalinda raia,   maafisa wa Congo na umoja wa mataifa walisema Alhamisi.

Butembo mji ambao kiini cha biashara wenye wakazi karibu milioni moja umekuwa kitovu cha ghasia za maandamano mabaya tangu mwezi uliopita ambapo darzeni za watu wameuwawa wakiwemo raia, walinda amani, na polisi wa congo.

Mamia ya wanajeshi na maafisa wa kiraia wameondoka mjini Butembo na majadiliano yamepangwa namna ya kuondoa vifaa vyao , gavana wa jimbo la kivu kaskazini Generali Constan Ndima amewaambia waandishi wa habari.

Msemaji wa MONUSCO Ndeye Khady Lo amesema kuondoka ni kwa muda. “ MONUSCO haiondoki Butembo baada ya mashauriano na maafisa wa ndani na kitaifa tume imesonga mbele na hatua ya maafisa wake kuondoka kwa muda, " aliliambia shirika la habari la Reuters, bila kusema lini watarejea.

Maandamano ambayo pia yametokea katika miji ya Goma na Uvira yamesababisha vurugu kwa walinda amani wa umoja wa mataifa ambao walipelekwa Congo kwa zaidi ya miongo miwili.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG