Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 20, 2025 Local time: 10:47

Ujumbe wa Baraza la Usalama la UN wafanya ziara nchini DRC


Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo

Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uko katika ziara ya siku nne nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kutathmini hali ya kisiasa nchini humo.

Kwa mujibu wa mwandishi wetu wa Kinshasa ujumbe huo utakuwa na mazungumzo na Rais Joseph Kabila, maafisa wa serikali, vyama vya upinzani na mashirika yasiyo ya kiserikali.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:40 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Msemaji wa tume ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa (MONUSCO), Felix Basse amesema kuwa ujumbe huo una ajenda nzito ikijumuisha juhudi kubuni suluhisho la mzozo wa kisiasa na hali ya usalama katika eneo la Kivu Kaskazini.

Vyama vya upinzani na baadhi ya mashirika ya kiraia ambayo hayakushiriki katika mazungumzo ya awali ya kisiasa nchini humo yamesema wanasubiri kwa hamu kukutana na ujumbe huo wa baraza la usalama.

XS
SM
MD
LG