Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 24, 2024 Local time: 22:42

MONUSCO yatazamia kurudisha ushirikiano na jeshi la DRC


Wanajeshi wa MONUSCO kwenye kituo cha ukaguzi.
Wanajeshi wa MONUSCO kwenye kituo cha ukaguzi.

Wasiwasi wa haki za binadam zilolazimisha MONUSCO kusitisha ushirikiano wao , unaweza kutatuliwa.

Afisi ya umoja mataifa huko jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, MONUSCO, inaeleza kuwa inatazamia kurejea kwa ushirikiano kamili wa kijeshi na jeshi la Congo. Mkuu mpya wa MONUSCO anatarajiwa kuwasili hivi karibuni.

Ofisi ya umoja mataifa nchini DRC ilisitisha kwa mda ushirikiano wao na jeshi la Congo, FARDC hapo February, baada ya majenerali wawili walotuhumiwa kwa unyanyasaji wa haki za binadam, kupewa jukumu la kuongoza kile kilicotakiwa kuwa operesheni ya pamoja ya FARDC na umoja matiafa, dhidi ya waasi wa FDLR.

Ikitaja sera za haki za bindam za umoja mataifa, ofisi hiyo, iliondowa uungaji mkono kwa operesheni hiyo, japo imeendelea kuunga mkono jeshi dhidi ya makundi mengine yenye silaha. Hapo jumamosi, waziri wa mawasiliano wa DRC , Lambert Mende, alisema serikali yake inasubiri kurejelea mazungumzo na mkuu mpya wa MONUSCO, Maman Sidikou, baada ya kile alichoelezea kuwa matatizo fulani walokabiliana nayo na Martin Kobler, mkuu wa MONUSCO aliyemaliza muda wake mapema mwezi huu.

Bw. Kobler alikuwa anahitlafiana na wakuu wa DRC, juu ya rekodi ya haki za binadam za jeshi lao, uhuru wa kujieleza na maandalizi ya uchaguzi.

Bw. Mende pia alisema serikali inataraji kwamba mkuu mpya wa MONUSCO atasikiliza zaidi malalamiko ya serikali, na kusema huwenda kusiwe na matatizo ya mawasiliano ya kimsingi kwa vile mkuu mpya wa MONUSCO Sidikou, anatokea Niger.

Kaimu msemaji wa MONUSCO, Charles Bambara, alielezea matamshi ya Mende juu ya ushirikiano wa kijeshi kuwa unatia moyo.

Bambara alisema ,wamekuwa wakitaka ushirikiano huu kwa mda sasa, na mambo yanakwenda kwenye njia muafaka. Tunafanya kazi kuhakikisha tashtiti zote zinasawazishwa ili ushirikiano huu utaweza kurejea haraka iwezekanavyo.

Wasiwasi wa haki za binadam zilolazimisha MONUSCO kusitisha ushirikiano wao , unaweza kutatuliwa. Bamabara alisema ofisi hiyo itaendelea kutekeleza kikamilifu sera za umoja mataifa juu ya haki za binadam.

Bambara anasema, Umoja mataifa una misingi, na misingi hiyo hayatabadilika kwa sababu ya kubalishwa mtu anayeyatekeleza.

Bambara pia alisema ofisi hiyo inajaribu kusukuma mbele utaratibu wa uchaguzi huko DRC, na inaiitisha serikali kuweka kando fedha zinazohitajika kwa tume huru ta uchaguziXS
SM
MD
LG