Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 05:06

Uchaguzi Mkuu Kenya: Usajili wa wapiga kura waanza rasmi


Wapiga kura wa Kibera, Nairobi, Kenya wakisubiri kujiandikisha.
Wapiga kura wa Kibera, Nairobi, Kenya wakisubiri kujiandikisha.

Shughuli za usajili wa wapiga kura nchini Kenya kwa ajili ya uchaguzi mkuu baadae mwaka huu zimeanza rasmi nchini humo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa idhaa ya Kiswahili, Collins Liberty mchakato huo wa usajili unatarajiwa kuchukua takriban mwezi mmoja.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya(IEBC) takriban wapiga kura milioni 6 watapata nafasi ya kushiriki uchaguzi mkuu ambao umepangwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Tume hiyo imesema itatumia vifaa vya kielektroniki 80,000 kusajili wapiga kura hao katika maeneo mbali mbali.

Mdau wa masuala ya uchaguzi Mombasa eneo la Mvita, Ali Hassan Mwakulonda amesema shughuli hiyo imeanza katika vituo mbali mbali.

Mwandishi wa VOA amesema wakenya kadhaa wameonekana katika vituo mbali mbali wakihakiki majina yao iwapo yapo katika orodha hiyo na wengine pia kujisajili upya.

Amesema kumekuwa na wito kwa wanawake kuwanyima wanaume haki zao za ngono ili kushinikiza kwamba wajisajili kupiga kura, japokuwa mama Zam Zam Muhammad anapinga hilo.

Shughuli ya kuwasajili wapiga kura imeaanza huku tume hiyo ikitarajiwa kupata makamishna wapya.

Makamishna ambao wapo chini ya mwenyekit, Isaack Hassan wamekubali kuondoka mamlakani kutokana na shinikizo la viongozi wa kisiasa waliotaka makamishna wapya katika tume hiyo.

XS
SM
MD
LG