Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 11:06

Bomu lauwa takriban watu 20 Mogadishu


Shambulizi la bomu kwenye hoteli Moja mjini Mogadishu kwenye picha ya maktaba.
Shambulizi la bomu kwenye hoteli Moja mjini Mogadishu kwenye picha ya maktaba.

Bomu kubwa la kwenye gari limelipuka Jumapili asubuhi kwenye bandari ya Mogadishu na kuuwa takriban watu 20 huku darzeni wengine wakibaki na majeraha.

Bomu kubwa la kwenye gari limelipuka Jumapili asubuhi kwenye bandari ya Mogadishu na kuuwa takriban watu 20 huku darzeni wengine wakibaki na majeraha. Kundi la wanamgambo la al–Shabab limedai kuhusika kwenye shambulizi hilo lililotokea kwenye lango la bandari na kusababisha uharibifu mkubwa.

Wakazi wa Mogadishu wanasema kuwa mplipuko huo ulisikika kote mjini huku picha za moshi mweusi zikienezwa kupitia mitandao ya kijamii. Msemaji kutoka utawala wa kieneo wa Mogadishu Abdifitah Omar Halane ameambia VOA Idhaa ya Kisomali kuwa wengi wa walioathiriwa ni raiya wa kawaida.

XS
SM
MD
LG