Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 22, 2024 Local time: 15:12

Moderna kupeleka chanjo zaidi Afrika kwa gharama nafuu


Chanjo ya moderna.
Chanjo ya moderna.

Moderna inasema itapeleka  hadi dozi milioni 110 za chanjo yake ya COVID-19  kwa nchi za Afrika

Moderna inasema itapeleka hadi dozi milioni 110 za chanjo yake ya COVID-19 kwa nchi za Afrika.

Tangazo hilo la Jumanne linasema Moderna iko tayari kutoa dozi milioni 15 za kwanza ifikapo mwisho wa mwaka huu, na milioni 35 katika robo ya kwanza ya 2022 na hadi milioni 60 katika robo ya pili. Inasema dozi zote zinatolewa kwa bei ya chini kabisa ya Moderna.

Kampuni hiyo iliiita hatua ya kwanza katika ushirikiano wao wa muda mrefu na Umoja wa Afrika, ambayo imekuwa wazi juu ya hitaji la dozi nyingi zaidi za chanjo ya COVID-19. Afrika na watu wake bilioni 1.3 wamesalia kuwa eneo lisilo na chanjo zaidi ulimwenguni dhidi ya COVID-19, na zaidi kidogo ya asilimia 5 tu ndio wamechanjwa kikamilifu.

Moderna ilisema makubaliano haya ni tofauti na makubaliano yake na mradi wa kimataifa wa COVAX wa kutoa hadi dozi milioni 500 kuanzia mwishoni mwa mwaka huu hadi 2022. COVAX inalenga kusambaza chanjo kwa nchi za kipato cha chini na cha kati.

XS
SM
MD
LG