Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 08:36

Mnyanyua vyuma raia wa Uganda aliyetoweka Japan afunguliwa mashtaka


Wanariadha wa Uganda kwenye ufunguzi wa mashindano ya Olimpiki mjini Tokyo, Japan.
Wanariadha wa Uganda kwenye ufunguzi wa mashindano ya Olimpiki mjini Tokyo, Japan.

Kijana huyo wa miaka 20 alipatikana siku kadhaa baadaye, na kusafirishwa hadi nchini Uganda ambapo maafisa wa serikali walisema, atapata ushauri nasaha.

Kijana mnyanyua vyuma wa Uganda aliyetoweka nchini Japan baada ya kukosa kufuzu kwa michuano ya Olimpiki mjini Tokyo, Japan, leo amefunguliwa mashtaka ya kula njama ya ulaghai, wakili wake amesema.

Julius Ssekitoleko, alitoweka kutoka kambi ya mazoezi ya Olimpiki, baada ya kujua hakutimiza viwango vya kushindana, kwenye Michezo hiyo, jina lake likigonga vichwa vya habari ulimwenguni kote, wakati maafisa wa Japan wakimtafuta. Kijana huyo wa miaka 20 alipatikana siku kadhaa baadaye, na kusafirishwa hadi nchini Uganda ambapo maafisa wa serikali walisema, atapata ushauri nasaha.

Lakini alichukuliwa haraka chini ya ulinzi wa polisi, na Jumatano alishtakiwa kwa "kula njama ya ulaghai" kabla ya kuachiliwa kwa dhamana ya polisi, wakili wake Anthony Wameli ameliambia AFP.

Msemaji wa idara ya upelelezi wa jinai nchini Uganda, alisema Ssekitoleko anaweza kuwa alikula njama na pamoja na afisa wa serikali, ili kujumuishwa kwenye timu ya kwenda Japan,

Familia ya Ssekitoleko ilikuwa imetoa rufaa ya kuachiliwa kwake, ikisema haki zake zinakiukwa.

XS
SM
MD
LG