Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 18:50

Mnangagwa amwita Mugabe baba wa taifa


Wananchi wa Zimbabwe waliohudhuria kwa wingi katika sherehe za kuapishwa Rais Emmerson Mnangagwa Harare, Zimbabwe, Novemba 24, 2017.
Wananchi wa Zimbabwe waliohudhuria kwa wingi katika sherehe za kuapishwa Rais Emmerson Mnangagwa Harare, Zimbabwe, Novemba 24, 2017.

Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa Ijumaa amemsifia Rais mstaafu Robert Mugabe na kuahidi kufanya uchaguzi mkuu mwaka 2018 kama ilivyokuwa imepangwa.

Mnangagwa amemwagia sifa Mugabe kwa kumwita "baba wa taifa letu" na kukiri kuwa rais mstaafu alifanya "makosa ya kukusudia na kutokusudia."

Kiongozi huyu mpya aliwaambia watu kwenye uwanja wa mpira wa taifa wenye viti 60,000 mjini Harare kuwa "jukumu kubwa mbele yetu ni kulijenga taifa letu kubwa mara nyingine.

Mnangagwa amesema kuwa yuko tayari kuwalipa wakulima ambao walipoteza ardhi yao chini ya utawala wa Mugabe.

Wapinzani wa Mugabe wamesema kuwa mgogoro wa programu ya marekebisho ya ardhi katika nchi hiyo iliwalazimisha wafanyabiashara wa kilimo wengi wao wenye uzoefu kuachia ardhi zao, na hilo kupelekea kuwepo njaa katika taifa hilo, nchi ambayo ilikuwa inazalisha chakula cha kutosha kusini mwa Afrika.

Mnangagwa alifukuzwa kutoka katika wadhifa wake wa naibu rais na aliyekuwa rais wa nchi hiyo na kuashiria kumuachia madaraka mkewe Grace. Sherehe hizo za kuapishwa kwake zilifanyika kwenye uwanja wa michezo mjini Harare na kuhudhuriwa na maelfu ya Wazimbabwe.

Kwa mujibu wa historia ya Zimbabwe, Mnangagwa anajulikana kama mamba ana uhusiano wa karibu na jeshi la nchi hiyo.

Pia duru za siasa zinaripoti kuwa Rais Mnangagwa atakabiliwa na mitihani mingi ya kuujenga tena uchumi wa nchi hiyo ambao umeharibika vibaya kutokana na utawala wamiongo minne ya Mugabe. Hata hivyo Mugabe pamoja na mkewe Grace Mugabe wamepewa kinga ya kutoshitakiwa.

XS
SM
MD
LG