Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 07, 2023 Local time: 03:04

Mnada wa chai Mombasa kufanyiwa mageuzi


Mnada wa chai Mombasa kufanyiwa mageuzi

Wakuu wa mnada wa chai huko Mombasa wanapanga kubadili mtindo wa biashara na kuanza kutumia komputa.

Kila Jumatatu na Jumanne, takriban madalali 80 na wanunuzi wanakutana pamoja katika jengo la kikoloni mjini Mombasa wanapatana bei, kwa njia ambayo ni nzuri kuhusu bei ya chai. Hiyo ni taasisi tangu enzi ya ukoloni inayojulikana kama Mombasa tea auction.

Mnada wa chai huenda ukaonekana kuwa ni jambo la kizamani, lakini kila mwaka inafanikiwa kupitisha takriban kilo milioni 345 za chai kutoka nchi tisa. Hii inafanya ni idadi kubwa ya kituo cha mnada wa chai duniani, kwa mujibu wa peter kimanga, mwenyekiti wa chama cha biashara ya chai Afrika Mashariki.

“Kanuni za utanashati zinafuatwa, kama vile kuvaa tai kwa madalali, hata katika eneo lenye hali ya hewa ya joto kama Mombasa na mashati ya kola kwa wanunuzi. Katika chumba cha mnada, wanaume wanaitana ‘Sir’ na licha ya kutokuwepo kwa vipaza sauti, ni mara chache utamsikia mtu yoyote akipaza sauti yake”.

Geoffrey rimbere, meneja wa mnada, anaelezea kwanini. Anasema kila mwaka wana warsha juu ya utanashati na itifaki katika chumba cha mnada. Huwezi kutumia lugha ambayo haikubaliki huko, au tabia ambayo si ya kawaida. Huo ndiyo utamaduni wa hapo. Huwezi kutumia lugha ambayo si nzuri. Hata kama hupati unachokitaka, bado unatakiwa uwe na adabu.

Sekta ya chai kenya unaweza kuiangalia kuanzia mwaka 1903 na asilimia 62 ya zao hilo linapandwa na wakulima wadogo wadogo. Mnada bado una hisia za zamani. Lakini kwa jinsi ulivyo katika kufuata taratibu, chai inauzwa haraka, wanauza kiasi cha shehena tano kwa dakika, na wanunuzi wanaangaliana kila mmoja kama vile wachuuzi.

Lakini yote haya yatabadilika, kwa vile mnada wa chai Mombasa unajitayarisha kuingia katika mtandao wa internet kibiashara ifikapo mwaka 2013. Mfumo wa zamani wa uuzaji wa chai utachukuliwa na mnada wa njia ya eletroniki ambapo wanunuzi watashiriki mnada kwa kutumia kompyuta zao, na siyo kuvutiana kila mmoja.

Rimbere anaelezea kwamba mabadiliko haya ni muhimu ili sekta hii iwe na kasi ya kusonga mbele. Mfumo wa mtandao utarekebisha mambo, anasema, utaruhusu madalali kuipeleka haraka haraka chai na kupunguza gharama za kuiweka katika ghala.

Bado, si kila mmoja anashawishika kwamba mabadiliko haya ni mazuri. Wanunuzi wengi, kama vile aweys mohammed, wana mashaka kwamba Mombasa ina miundo mbinu muhimu ya kufanya kazi ya kuuza mnada kwa njia ya mtandao, na wanakhofia athari zake zitajitokeza kwa uchumi wa ndani.

“Mawasiliano ya internet hapa nchini ni mabaya sana,. Nini kitatokea utakapokuwa unashiriki katika baadhi ya mnada na mara mawasiliano yanakatika? Kitu gani kitawatokea baadhi ya wateja? Wanaweza kushiriki mnada popote. Kitu gani kitatokea kwa maslahi ya makampuni ya ndani ambayo yanaajiri watu ambao walikuwa wakijishughulisha na biashara hii?”

Upande mwingine wa mtaa kutoka kwenye eneo la mnada, kuna jengo moja la zamani, ambako kuna kampuni ya africa tea brokers, kampuni kubwa kabisa ya uuzaji chai nchini kenya. mkurugenzi wake, tom muchura anaonja mamia ya sampuli za chai kila wiki, akielezea ladha, rangi na nguvu ya kila aina moja ya chai kabla ya kuipeleka mnadani.

“Unachukua kiasi kidogo tu unakionja. Halafu unaizungusha ndani yam domo hiyo chai halafu ukishapata ladha yake unaitema. Kwa kweli unatuona tunaonja mpaka vikombe 250 vya chai kwa wakati mmoja, na mtu anaweza kuona tofauti kati ya kila kikombe unachoonja”.

Muchura amekuwa akifanya kazi kwenye africa tea brokers kwa zaidi ya miaka 40, na mnada wa njia ya mtandao si moja ya mabadiliko makubwa aliyoyaona. Sekta hiyo yenye imeenea kote afrika mashariki anasema na mahitaji yameongezeka, hasa katika nchi za kiislamu.

Lakini anasema mfumo wa mnada kwa njia eletroniki kwa hakika utabadili jinsi madalali na wanunuzi wanavyowasiliana. Muingiliano muhimu kisaikolojia, utapotea, lakini ni kipindi cha mpito ambacho kwa hakika hakiepukiki.

XS
SM
MD
LG