Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 19:33

Waomboleza mauaji ya mtu mweusi Louisiana


Waombolezaji waliobeba mishumaa walikusanyika jana Jumatano kwa sala iliyofanyika nje ya duka la Baton Rogue, katika jimbo la Louisiana, pahali ambapo mwanaume mmoja Mmarekani mweusi alipigwa risasi na kuuawa na polisi chini ya saa 24 zilizopita, tukio ambalo lilinaswa kwenye video kupitia simu ya mkono na ambalo limeibua mjadala wa kitaifa kuhusu matumizi ya nguvu dhidi ya Wamarekani weusi na jamii zingine za walio wachache hapa Marekani.

Picha ya Alton Sterling alipouawa na polisi, July 5, 2016.
Picha ya Alton Sterling alipouawa na polisi, July 5, 2016.

Umati mkubwa wa watu ulionekana nje ya duka la Triple S Mart kwa siku nzima kupinga kifo cha Alton Sterling mwenye umri wa miaka 37, huku wakibeba mabango yaliyoandikwa “Maisha ya watu weusi ni muhimu pia” na “Mikono juu…Usifytue risasi”, jumbe ambazo zimetumika hapo awali kufuatia maafa yaliyotokana na makabiliano kati ya polisi na wakaazi ambao ni Wamarekani weusi.

XS
SM
MD
LG