Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 22, 2025 Local time: 13:02

Mlori yaanza kuingia Gaza kupitia Israel


Malori ya misaada yaliingia Gaza kutoka kusini mwa Israel, Jumapili kupitia makubaliano mapya ya kutotumia kivuko cha  Rafah na Misri baada ya wanajeshi wa Israel kuukamata  upande wa Wapalestina mapema mwezi huu.

Lakini haikuwekwa wazi kama makundi ya kibinadamu yataweza kupata misaada kwa sababu ya mapigano yanayoendelea katika eneo hilo.

Misri inakataa kufungua tena upande wake wa mpaka wa Rafah hadi udhibiti wa upande wa Gaza utakaporejeshwa kwa Wapalestina.

Ilikubali kuelekeza misafara kwa muda kupitia mpaka wa Kerem Shalom wa Israel, ambacho ni kituo kikuu cha mizigo kwa Gaza, baada ya mazungumzo kati ya Rais wa Marekani, Joe Biden na Rais wa Misri Abdel-Fattah el-Sissi.

Lakini kivuko hicho kwa kiasi kikubwa hakipitiki kwa sababu ya mapigano yanayohusishwa na mashambulizi ya Israel katika mji wa karibu wa Rafah.

Forum

XS
SM
MD
LG