Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 11:06

Mlipuko wauwa wawili Kigali


Harakati za usafiri katika mji wa Kigali, Rwanda
Harakati za usafiri katika mji wa Kigali, Rwanda

Mlipuko wa bomu katika barabara ya kwenda uwanja wa ndege mjini Kigali wauwa watu wawili na wengine karibu 30 kujeruhiwa.

Mlipuko wa bomu Ijumaa magharibi mjini Kigali umeuwa watu wawili na wengine 28 kujeruhiwa. Mlipuko ulitokea majira ya saa moja jioni katika barabara kuu kutoka uwanja wa ndege kuelekea katikati ya mji wa Kigali.

Msemaji wa polisi Theos Badege aliwaambia waandishi wa habari kuwa kati ya watu 28 waliojeruhiwa, 10 wako mahututi. Hakuna aliyedai kuhusu katika shambulio hilo mara moja, lakini polisi wanasema wamewatia nguvuni watu wawili kwa mashaka kuwa wanahusika katika mlipuko huo.

Hali ya taharuki iliingia mjini Kigali ijumaa jioni baada ya mlipuko huo na kusababisha watu kukimbia huku na huko.

Mwezi Februari mwaka jana Kigali ilipigwa na mfululizo wa milipuko ya mabomu ya namna hii.

XS
SM
MD
LG