Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 15:09

Mlipuko wauwa watatu Mombasa


Mji wa Mombasa majira ya usiku
Mji wa Mombasa majira ya usiku

Polisi wanasema gruneti hilo lilirushwa katika kundi la watu waliokuwa wakiangalia mechi ya mpira

Idadi ya watu waliokufa kufuatia mlipuko wa Grunedi mjini Mombasa huko Kenya Jumapili usiku, imeongezeka na kufikia watu watatu.

Mlipuko huo ulitokea saa tatu usiku katika baa moja iliyo mtaa wa Mshomoroni, viungani mwa jiji la Mombasa. Maafisa wa usalama huko mkoani Pwani wanaendelea na uchunguzi kufuaita shambulio hilo, huku wakiwatafuta watu waliohusika.

Afisa mkuu wa polisi mkoani Pwani Aggrey Adoli amethibitisha uvamizi huo, ambapo gunedi ilirushwa katika umati wa watu waliokuwa wakitazama mechi ya kandanda usiku.

Waliofariki ni wanaume watatu akiwemo mtoto aliye na umri wa miaka 9, na majeruhi wengine bado wanatibiwa hospitali mjini Mombasa. Watu kadhaa kutoka kijiji cha Mshomoroni wameeleza kile walichoshuhudia, kuhusiana na tukio hilo.

Shambulio hilo linalosusishwa na tendo la ugaidi limetokea siku moja tu baada ya ubalozi wa Marekani kuonya raia wake kuhusu uwezekano wa magaidi kushambulia Mombasa.
Serikali ya Marekani ilitangaza kusitisha safari zote katika pwani ya Kenya hadi Julai mosi, hatua ambayo ilikosolewa na baadhi ya viongozi nchini Kenya wakisema ni pigo katika sekta ya utalii.

XS
SM
MD
LG