Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 23:17

Mlipuko watokea Nagorno-Karabakh


Mlipuko mkubwa ulitikisa eneo la milima la Nagorno-Karabakh Jumatatu jioni wakati Waarmenia wa kabila hilo wakimiminika kutoka eneo hilo lililojitenga baada ya jeshi la Azerbaijan kuchukua udhibiti kamili wa eneo wiki iliyopita.

Mlipuko huo katika kituo cha kuhifadhi mafuta karibu na mji mkuu wa mkoa, Stepanakert, ulijeruhi zaidi ya watu 200, mchunguzi wa haki za binadamu wa Nagorno-Karabakh, Gegham Stepanyan amesema kwenye mtandao X, ambao zamani ulijulikana kama Twitter.

Haijafahamika mara moja ni nini kilisababisha mlipuko huo, wakati wananchi wakipanga foleni kutafuta mafuta ya magari ili kuondoka mkoani humo.

Wengi wa waathirika walikuwa katika hali mbaya, Stepanyan alisema, akiongeza kuwa watahitaji kusafirishwa kwa ndege kutoka eneo hilo kwa matibabu ili kuokoa maisha yao. Haikuweza kufahamika mara moja iwapo kulikuwa na vifo vyovyote.

Forum

XS
SM
MD
LG