Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 30, 2020 Local time: 08:33

Mlipuko wavunja jengo la UN Nigeria


Wafanyakazi za uokozi wakijaribu kuokoa watu au kutoka maiti katika jengo la Umoja wa Mataifa Abuja Augusti 26, 2011.

Watu wasiopungua 16 mpaka sasa inasemekana wamekufa katika mlipuko huo kwenye jengo la ofisi za Umoja wa Mataifa

Mlipuko wa bomu katika jengo lenye ofisi za Umoja wa Mataifa katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, umeuwa watu wasiopungua 16, huku ripoti zikisema huenda idadi hiyo ikaongezeka.

Mashahidi wanasema ilionekana gari iliyojigongesha katika jengo hilo lenye ghorofa nne na kulipuka.

Umoja wa Mataifa umethibitisha mlipuko huo ambao ulitokea majira ya saa tano asubuhi kwa saa za Nigeria.

Mashahidi wanasema wafanyakazi za uokozi walikimbilia kutoka watu walionusurika na maiti kutoka katika kifusi cha jengo hilo.

Ripoti zinasema karibu watu 400 wanafanya kazi katika jengo hilo ambalo liko karibu na majengo mengine ya kibalozi, ikiwa ni pamoja na ubalozi wa Marekani.

Hakuna ambaye amedai kuhusika na shambulizi hilo mpaka sasa.

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG