Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 19:45

Mlipuko wa guruneti wauwa watu 3 Kenya


Basi la abiria lililoripuliwa kabla ya kuelekea Kampala, Juamtatu 20/12/2010
Basi la abiria lililoripuliwa kabla ya kuelekea Kampala, Juamtatu 20/12/2010

Polisi nchini Kenya wanasema bomu lililokuwa ndani ya gari lilipuka pembeni ya basi huko Nairobi na kuuwa watu wapatao watatu na kujeruhi wengine 26.

Maafisa wanasema bomu hilo lilipuka wakati abiria wakijitayarisha kupanda basi ambalo lilikuwa linatarajiwa kwenda Kampala Uganda.

Polisi wanasema abiria aliokuwa amebeba begi hilo lenye mabomu alipogundua mapolisi wanapekuwa mizigo yote alitupa begi hilo na kujaribu kukimbia.

Ni mmoja wa waliofariki dunia.

Mkuu wa Polisi wa Uganda alionya Jumatatu juu ya uwezekano wa vitisho vya kigaidi kutoka kwa alqaida na makundi mengine ya kiislam yenye msimamo mkali ikiwa ni pamoja na Al Shabab ya Somalia wakati wa sherehe za Krismas.

XS
SM
MD
LG